Course Overview
Maelezo ya Kozi:
Katika dunia ya teknolojia inayokua kwa kasi, simu za mkononi zimekuwa zana muhimu katika uandishi wa habari. Kozi hii itawezesha wanafunzi kuelewa na kutumia simu zao katika upigaji picha, uandaaji wa video, na uandishi wa sauti. Pia, itakazia jinsi ya kuhariri na kuwasilisha taarifa kwa kutumia programu mbalimbali za simu.
Mafunzo yatakayopatikana:
- Upigaji Picha kwa Kutumia Simu: Maelezo ya msingi ya upigaji picha na simu.
- Vitu vya Kuzingatia Wakati wa Kupiga Picha: Taa, umbali, na maandalizi ya kupiga picha.
- Jinsi ya Upigaji Picha: Kupanga na kutumia kamera ya simu.
- Umbali Katika Upigaji Picha: Kuzingatia umbali kwa matokeo mazuri.
- Vifaa vya Kuzingatia Katika Kupiga Picha: Kuchagua vifaa kama tripod na lensi.
- Zifahamu Programu za Kutumia Wakati wa Kupiga Picha: Kutumia Snapseed, Lightroom, na VSCO.
- Jinsi ya Kurekodi Video Kwa Kutumia Simu: Maelezo ya msingi ya uandaaji wa video.
- Uhariri wa Video (Video Editing) kwa Kutumia Programu za Simu: Kutumia iMovie, Adobe Premiere Rush, na Kinemaster.
- Vifaa Vinavyotumika Wakati wa Kurekodi Video kwa Kutumia Simu: Kuchagua vifaa sahihi kwa uandaaji wa video.
- Programu Nyepesi za Kuhariri Video Ndani ya Simu Yako: Uelewa wa programu rahisi za uhariri wa video.
- Vitu vya Kuzingatia Wakati wa Kurekodi Sauti: Maandalizi na mazingira sahihi ya kurekodi sauti.
- Mbinu bora za Uhariri wa Sauti (Audio): Uhariri wa sauti kwa kutumia programu za simu.
Lengo la Kozi:
Wanafunzi watakuwa na uwezo wa kuzalisha taarifa za habari zenye ubora wa juu kwa kutumia simu zao. Watajifunza jinsi ya kuzalisha picha, video, na sauti zenye ubora, na jinsi ya kuhariri na kuzipanga kwa kutumia programu za simu.
Kwa nini Ujiandikishe?:
Kama unataka kuwa mwandishi wa habari wa kisasa anayeweza kufanya kazi kwa kutumia simu yake, kozi hii ni muhimu kwako. Jisajili sasa na anza safari yako ya uandishi wa habari wa kidigitali!
Muhibu Kamlete
Thank you
Mario
Nashukuru sana kwa mafunzo yenu
Furahisha Hekima Nundu
Nashukuru kwa kozi hii muhimu naamini itasaidia katika kukuza tasnia na ubira wa Habari
Said Sindo
Niwashukuru sana the Click Institue kwa mafunzohaya. Yameniongezea umahiri katika uandishi wangu wa habarihasa kwa kutumia simu janja. Asante Mwalimu Suedi, sitokuangausha.
Nasra Denis
Hongera sana mwalimu ,hakika masomo ni mazuri sana nimeongeze ujuzi WA kutumia simu Katika kuchukua matukio na kuhariri
Alodia Dominick
Nashukuru sana mafunzo ni mazuri
Alodia Dominick
Nashukuru sana mafunzo ni mazuri
Ila yaingie kwa udani zaidi ili tuweze kupata uelewa mpana
Alodia Dominick
Nashukuru sana mafunzo ni mazuri, nimefurahi kupata uelewa wakati wa kupiga picha vitu vya kuzingatia, taa, umbali na kufanya maandalizi ya kupiga picha. Lakini pia jambo jingine kwenye kupiga picha lazima uchague ni vifaa gani utavitumia mfano, tripod na lensing.
Kuna kitu kingine ambacho nimeelewa kuwa wakati wa kupiga picha kuna program zinatumika kama snapped, right room na visco
Katika kuhariru video unatumia Adobe premier, rush na Kinemaster.
Angela Batuli Sebastian
Masomo ni mazuri wakati mwingine naomba yaeleze kwa undani zaidi,ninejifunza namna ya kupiga picha kwa kutumia camera ya simu,kuzingatia umbali ili kuleta matoke mazuri,kurecodi video kwa kutumia simu maelezo ya msingi,kuandaa vifaa sahii unapotaka kuchukua video na kuzifahamu program za kutumia wakati wa kupiga picha.
Veronica Mrema
Kozi ilikuwa nzuri sana.
Rabia Nandonde
Mafunzo ni mazurii mnooo
Pendo Laizer
Kozi ilikuwa nzuri
Pendo Laizer
Kama ikiwezekana tukutane wote ana kwa ana tuisome kozi zaidi
Asiyejulikana
Course nzuri sana asanteni wakufunzi
ASIA KILAMBWANDA
Kuelewa namna mzuri ya upigaji picha kwa kutumia simu.
Anjela Sebastian
Asante kwa mafunzo mazuri nimetoka na jambo nimejifunza namna ya kutumia vifaa mbalimbali wakati ninapotumia simu yangu kurecodi video au kupiga picha mfano tripod na attachment,mambo ya kuzingatia wakati narecod sauti kwa kutumia simu ,orientation namna gani unapiga picha,landscap yaani mlalo ili kuweza kuchukua tukio kwa ukubwa au wingi na Potrate kuchukua kwa useful zaidi na mengine mengi.
Sophia kingimali
Asante mwl kwa mafunzo haya ni mazuri
Khalphani Bakari
Thanks
Asha Kazambo
Nashukuru kwa mafunzo mazuri ambayo yanatujenga sisi kama waandishi wa habari katika kuhakikisha vifaa tunavyovitumia katika tasnia yetu ya uandishi wa habari vinafanya kazi kwa usahihi ili kufikisha maudhui kwa jamii kama yalivyokusudiwa.
Lukia Chasanika
Kuhariri picha na upigaji wa picha pamoja na kurekodi video
mary sanyiwa
upigaji picha kwa kutumia simu
Arodia Peter
kozi hizi ni nzuri, zinatuongezea uelewa wa mambo mengi kuhusu namna ya kuandika, kupiga picha na kuhariri picha.
Arodia Peter
kozi zote nzuri
FARIDA MANGUBE
Kozi nzuri
Hadija Omary
Somo zuri Sana limenikumbusha vitu vingi