Course Overview
Maelezo ya Kozi: Kozi hii inalenga kubadilisha mtazamo wa wanafunzi kuhusu mahojiano katika uandishi wa habari. Sio tu kuhusu kuuliza maswali, bali pia kujenga mazingira ambayo mwandishi na mhojiwa wanashiriki kwa kina na uaminifu. Kozi hii inaweka msisitizo mkubwa katika kuunda mahojiano yenye maudhui na kuleta taarifa zenye thamani kwa wasomaji na watazamaji.
Unachotarajia Kujifunza:
- Fahamu Zaidi Kuhusu Mahojiano: Elewa kwa kina historia, aina, na mbinu mbalimbali za mahojiano ili kuongeza tija katika mazungumzo.
- Maandalizi ya Mahojiano: Pata mwongozo wa kina kuhusu jinsi ya kutafiti, kupanga na kujitayarisha kwa mahojiano ili yawe na mafanikio makubwa.
- Mambo ya Kuzingatia Wakati wa Mahojiano: Jifunze kuhusu jinsi ya kuheshimu wapiga picha, mhojiwa, na wasikilizaji kwa kuzingatia maadili ya kitaaluma.
- Jinsi ya Kuuliza Maswali: Master mbinu za kuuliza maswali yanayochimba kwa kina na kufungua mazungumzo yenye tija.
Matarajio: Baada ya kumaliza kozi hii, utakuwa:
- Na ujuzi wa kina kuhusu mahojiano na jinsi ya kuyafanya yawe na tija.
- Uwezo wa kuandaa na kuendesha mahojiano yenye mafanikio.
- Na ujuzi wa kuheshimu maadili ya kitaaluma wakati wa mahojiano.
Vifaa vya Mtandaoni: Kozi hii inatumia teknolojia za kisasa kutoa mafunzo. Kutakuwa na video za kufundishia, mifano ya mahojiano halisi kutoka kwa wataalam wa habari, na majukwaa ya majadiliano ambapo wanafunzi wanaweza kubadilishana mawazo na wenzao, kufanya mazoezi na kujifunza kwa vitendo.
Kwa nini Ujiandikishe? Kozi hii siyo tu itakupa ujuzi wa mahojiano, bali pia itakusaidia kujenga ujasiri na kuboresha ujuzi wako wa mawasiliano. Kama unataka kufikia kiwango cha juu katika uandishi wa habari na kuwa na uwezo wa kufanya mahojiano yatakayoacha alama, hii ndiyo kozi yako. Jisajili leo na anza safari yako ya kubadilisha jinsi unavyoendesha mahojiano!
Sabra ali pandu
Jinsi ya kufanya mahojiano katika uandishi wa habari
Kennneth Ngelesi
Mahojiano
PIERRE HAKIZIMANA
I love it,
It’s very helpful and clear
NEEMA MTUKA
MAHOJIANO
Pendo Laizer
Kozi nzuri
Nasra Denis
Nimejifunza kwa usahihi namna ya kufanya mahojiano
Anjela Sebastian
Nimejifunza jinsi ya kufanya mahojiano asante Temi mafunzo ni mazuri
Hilda Kinabo
Kozi ni nzuri sana na imenisaidia kuelewa mambo mengi muhimu katika kazi yangu